Avito wa Vienne
From Wikipedia, the free encyclopedia
Avito wa Vienne (kwa Kilatini: Alcimus Ecdicius Avitus; Vienne, Ufaransa, 450 hivi – 5 Februari 523) alikuwa mshairi halafu askofu mkuu wa mji huo kuanzia mwaka 494.
Ni maarufu kwa imani na juhudi zake ambazo aliweza kumaliza Uario kati ya Waburgundi na kuwavuta katika Kanisa Katoliki, pamoja na kukinga Galia nzima dhidi ya uzushi huo.
Baba yake alikuwa seneta, halafu askofu wa Vienne. Vilevile mdogo wake Apolinari alipata kuwa askofu wa Valence.
Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Februari[1].