From Wikipedia, the free encyclopedia
Augustine Philip Mahiga (28 Agosti 1945 - 1 Mei 2020) alikuwa mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha siasa cha CCM.
Aliteuliwa kuwa mbunge na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa miaka 2015 – 2020 na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. [1] Tarehe 3 Machi 2019 alihamishwa kwenye Wizara ya Sheria na Katiba kwa kubadilishawa nafasi na Palamagamba Kabudi aliyepelekwa Wizara ya Mambo ya Nje kutoka ile ya Sheria.
Aliwahi kuwakilisha Tanzania akiwa balozi kwenye Umoja wa Mataifa kati ya miaka 2003 hadi 2010. Kati ya 2010 hadi 2013 aikuwa mkuu wa ofisi ya UM kwa Somalia.
Mahiga alikuwa na elimu ya ualimu (BA kutoka UDSM 1970), akaendelea kusoma Kanada alipohitimu shahada ya uzamivu katika mahusiano ya kimataifa kwenye Chuo Kikuu cha Toronto mwaka 1975. Mwaka 1977 aliingia katika utumishi wa serikali akiajiriwa katika ofisi ya rais. Tangu mwaka 1983 alifanya kazi ya balozi wa Tanzania kwenye vituo mbalimbali.
Aliaga dunia tarehe 1 Mei 2020 mjini Dodoma baada ya kuwa mgonjwa kwa muda mfupi. Sababu ya kifo haijatangazwa.[2][3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.