![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/13/Athalia.jpg/640px-Athalia.jpg&w=640&q=50)
Atalia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Atalia (kwa Kiebrania: עֲתַלְיָה, ʻĂṯalyâ, "Mungu anainuliwa"[1]) alikuwa malkia wa ufalme wa Yuda kama mke wa mfalme Yehoramu wa Yuda, aliyekuwa wa ukoo wa David.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/13/Athalia.jpg/320px-Athalia.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/57/Athaliah1.jpg/320px-Athaliah1.jpg)
Baada ya huyo kufa, alijitwalia madaraka kinyume cha taratibu na kwa ukatili mkubwa (2Fal 11:1)[2] akatawala miaka 841–835 KK, mpaka alipopinduliwa na kuuawa (2Fal 11:14-16; 2Nya 23:12-15).
Binti au dada wa mfalme Ahabu wa Israeli, alijitahidi kueneza ibada kwa Baali na miungu mingine dhidi ya YHWH, Mungu pekee wa dini ya Musa.