Ashraf Ghani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ashraf Ghani Ahmadzai (kwa Kipashto: محمد اشرف غني احمدزی / kwa Kidari: محمد اشرف غنی احمدزی; alizaliwa 19 Mei 1949) ni mwanasiasa, msomi, na mchumi wa Afghanistan ambaye alihudumu kama Rais wa Afghanistan.
Tarehe 15 Agosti 2021 alikimbia nchi wakati Taliban walielekea kuingia mji mkuu, Kabul. Alifika Falme za Kiarabu alipopewa hifadhi.[1][2] Makamu wake Amrullah Saleh alitangaza kwamba amechukua nafasi yake kufuatana na katiba ya nchi.[3]