Aruba
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Aruba ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi karibu na pwani ya Venezuela.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Kisiwa chenye heri" | |||||
Wimbo wa taifa: Aruba Dushi Tera | |||||
Mji mkuu | Oranjestad | ||||
Mji mkubwa nchini | Oranjestad | ||||
Lugha rasmi | Kiholanzi, Papiamento1 | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba | ||||
Uhuru |
|||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
178.91 km² () - | ||||
Idadi ya watu - 2018 kadirio - Msongamano wa watu |
116,600 (ya 193) 624/km² (ya 22) | ||||
Fedha | Florini ya Aruba (AWG2 ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AST (UTC-4) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .aw | ||||
Kodi ya simu | +297
- |
Tangu mwaka 1636 ilikuwa kwa kwikwi koloni la Uholanzi, lakini sasa ni "nchi ya kujitawala" ndani ya muundo wa "Ufalme wa Nchi za Chini" pamoja na Uholanzi yenyewe na nchi nyingine mbili za Karibi zilizokuwa makoloni ya Uholanzi.
Watu wa Aruba walielekea kwenye uhuru kamili wa kisiasa katika miaka ya 1980 na ya 1990.
Mwaka 1986 ilipata madaraka yote ya kujitawala chini ya taji la Uholanzi. Uhuru kamili ulipangwa kwa mwaka 1996 lakini serikali ya Aruba iliomba kutoendelea na mpango huo.
Wakazi ni 116,600 (2018); kwa asilimia 75 ni mchanganyiko wa Waindio, Wazungu na pia Waafrika. Watumwa Waafrika hawakuwa wengi jinsi ilivyo kwenye visiwa vingi vya Karibi kwa sababu kisiwa hicho hakikuwa na mashamba mengi ya miwa kutokana na ukame wa mahali. Hivyo sasa wenye asili hiyo ni 15% tu.
Wengi wao wanaongea Kipapiamento (68.3%) pamoja na Kihispania (13.5%), Kiingereza (7%) na Kiholanzi (lugha rasmi; 6%).
Upande wa dini, 75.3% ni Wakatoliki, 4.9% Waprotestanti n.k.
Aruba travel guide kutoka Wikisafiri
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aruba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.