Antonino wa Piacenza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Antonino wa Piacenza (alifariki Piacenza, 303) alikuwa Mkristo aliyeuawa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma chini ya kaisari Dioklesyano[1][2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Septemba[3].