Alfonso wa Orozco
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alfonso wa Orozco, O.S.A. (Oropesa, Toledo, Hispania, 17 Oktoba 1500 - Madrid, Hispania, 19 Septemba 1591) alikuwa padri wa shirika la Waaugustino aliyepata umaarufu kwa mahubiri yake na kwa maisha ya kiroho.
Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Januari 1882, halafu Papa Yohane Paulo II akamtangaza mtakatifu tarehe 19 Mei 2002[1].
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[2].