From Wikipedia, the free encyclopedia
Ala ya muziki ni kifaa kinachotoa sauti zinazotumiwa katika muziki. Kila ala ya muziki inatoa mitetemo katika hewa inayoendelea kusambaa na kupokewa na masikio kama sauti.
Kimsingi kila kitu kinachotoa sauti kinaweza kutumiwa kama ala ya muziki, lakini kwa kawaida jina hili linatumika kwa vitu vilivyotengenezwa hasa kwa shabaha hii. Wakati mwingine hata sauti ya binadamu inatajwa kama ala ya muziki.
Kuna aina nyingi za ala za muziki. Mara nyingi zinaainishwa na kutajwa kutokana na mbinu zake za kutoa sauti:
Wengine hutofautisha ala za muziki kutokana na namna ya matumizi, kama vile kupiga, kupuliza hewa, kupiga vibanzi au funguo (keyboard), kuchulia waya.
Kila jamii na kila utamaduni kwenye dunia imewahi kubuni ala zake za pekee.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ala ya muziki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.