Afro-Shirazi Party (kifupisho: ASP) kilikuwa chama cha siasa cha Zanzibar. Kilianzishwa mwaka 1957 kwa muungano kati ya Shirika la Washirazi (Shirazi Association) na Shirika la Waafrika (African Association). Shirika la Shirazi (lililoanzishwa 1939) lilikuwa muungano wa Waafrika wazalendo wa Unguja na Pemba, Shirika la Waafrika (lililoanzishwa 1934) muungano wa Waafrika wenye asili ya bara, pamoja na asili kati ya familia za watumwa wa awali kutoka bara na wafanyakazi waliohamia katika karne ya 20.

Thumb
Kanga ikitangaza TANU na ASP (makumbusho ya House of Wonders, Stone Town, Zanzibar).

Chama kilikuwa na wafuasi wengi kisiwani Unguja, ilhali sehemu ya Washirazi wa Pemba walipigia kura vyama vingine.

Katika uchaguzi kabla ya uhuru mwaka 1963 ASP ilipata asilimia 54.2 za kura lakini, kutokana na mfumo wa uchaguzi, haikupata wabunge wengi, hivyo serikali ya kwanza baada ya ukoloni ilianzishwa na vyama vya ZNP na ZPFP.

Katika Januari wa 1964 kikundi cha wana ASP wenye silaha kilichoongozwa na John Okello ilipindua serikali ya Sultani wa Zanzibar pamoja na kuua wakazi wengi Waarabu na Wahindi na kuunda serikali ya kimapinduzi chini ya urais wa Abeid Karume[1].

Mwaka wa 1977, ASP iliungana na TANU kuwa Chama cha Mapinduzi.

Tanbihi

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.