Abdulaziz I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Abdulaziz I au Abd Al-Aziz (9 au 18 Februari 1830 - 4 Juni 1876) alikuwa Sultani wa 32 wa Milki ya Osmani. Alikuwa mwana wa Sultani Mahmud II. Madarakani, alimfuata kaka yake, Sultani Abdulmecid I tarehe 25 Juni 1861.
Mwaka wa 1867 alipewa cheo cha "Sir" cha Uingereza.
Aliondoshwa madarakani na mawaziri wake tarehe 30 Mei 1876 na kugunduliwa akiwa amefariki siku tano baadaye. Haijulikani kama alijiua au aliuawa.