Tessa Thompson
Mwigizaji wa Marekani / From Wikipedia, the free encyclopedia
Tessa Lynne Thompson (alizaliwa Los Angeles[1], Kalifornia, Oktoba 3, 1983) ni mwigizaji wa filamu wa Marekani.
Alianza kazi yake ya kuigiza akiwa pamoja na kampuni ya wanawake ya Los Angeles ya Shakespeare akiwa anasoma katika Chuo cha Santa Monica, aliigiza kwenye filamu ya maonyesho kama The Tempest na Romeo na Juliet. Alipata mafanikio na umaarufu baada ya kuigiza kwenye filamu ya Mississippi Damned (2009) akiigiza kama Tina Mabry na kwenye filamu ya Tyler Perry's For Colored Girls (2010).
Thompson alipata umaarufu na kufahamika kupitia vichekesho vilivyojulikana kama Dear White People (2014), na aliigiza kama Diane Nash mwanaharakati wa haki za raia katika igizo la kihistoria la Ava DuVernay Selma (2014). Alipata pia umaarufu kwa kuigiza kama Bianca Taylor kwenye filamu ya Creed (2015) Creed II (2018) na Creed III (2023). Pia aliigiza kama Valkyrie katika filamu za Marvel Cinematic Universe, ikiwa ni pamoja na Thor: Ragnarok (2017) na Thor: Love and Thunder (2022), pamoja na kua mwigizaji mkuu katika filamu ya Men in Black: International (2019). Alipokea sifa katika filamu za kujitegemea alizoigiza ambazo zilikua kama Sorry to Bother You (2018), Annihilation (2018), Sylvie's Love (2020), and Passing (2021), na baadae aliteuliwa kuwania tuzo za Filamu za British Academy Film Award.