Mtindo wa Kigothi mamboleo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mtindo wa Kigothi mamboleo (kwa Kiingereza: Gothic Revival architecture, Victorian Gothic, neo-Gothic, au Gothick) ulikuwa mtindo wa usanifu majengo ambao uliiga kwa kiasi tofauti ule wa Kigothi uliotawala Ulaya katika karne za kati.
Mtindo huo ulianza Uingereza mwishoni mwa miaka ya 1740, ulistawi mwanzoni mwa karne ya 19, na kutawala katika ustaarabu wa Magharibi katikati ya karne hiyo.
Mfano maarufu katika Afrika Mashariki ni kanisa kuu la Mt. Yosefu (kwa Kiingereza: St Joseph Cathedral church) jijini Dar es Salaam, Tanzania, lililojengwa kwa umahiri na wamisionari Wabenedikto kutoka Ujerumani kuanzia mwaka 1897 hadi 1902[1] likatabarukiwa mwaka 1905.[2]. Hadi sasa ni kanisa kuu la Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kati ya sifa zake, mojawapo ni vioo vya rangi nyuma ya altare[3].