Mmisionari

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mmisionari

Mmisionari (au Mwanamisheni) ni mtu wa dini fulani ambaye anafanya kazi ya kuieneza kwa wasio waumini wa dini hiyo. Kwa kawaida mhusika ni Mkristo, lakini si lazima.

Thumb
Wamisionari Wakatoliki huko Papua New Guinea.

Jina linatokana na neno la Kilatini missio lenye maana ya utume (kutuma au kutumwa).[1]

Mara nyingi, kazi hiyo inakwenda sambamba na utoaji wa huduma za kijamii, hasa elimu, afya, utetezi wa haki[2], maendeleo katika uchumi n.k.[3][4]

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.