Mwanasheria wa Kislovakia, mwanaharakati wa mazingira na mwanasiasa From Wikipedia, the free encyclopedia
Zuzana Čaputová (alizaliwa 21 Juni 1973) ni mwanasiasa, wakili na mwanaharakati wa mazingira kutoka Slovakia. Ni rais wa tano wa Slovakia, nafasi ambayo ameshikilia tangu 15 Juni 2019. Čaputová ndiye mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa urais, vilevile rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Slovakia, aliyechaguliwa akiwa na umri wa miaka 45.[1]
Čaputová alijulikana kwa mara ya kwanza kwa kushinda katika mapambano ya muongo mzima dhidi ya dampo lenye sumu katika mji wake wa Pezinok. Kwa hili, Čaputová alipewa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mwaka 2016. Alishinda uchaguzi wa urais wa Slovakia wa 2019 kwa 58% ya kura katika duru ya pili.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.