From Wikipedia, the free encyclopedia
Zubani Shimali (kwa Kilatini na Kiingereza: Zubeneschamali; pia α Beta Librae, kifupi Beta Lib, α Lib) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Mizani (Libra).
(Beta Librae, Zubeneschamali) | |
---|---|
Kundinyota | Mizani (Libra) |
Mwangaza unaonekana | 2.61 |
Kundi la spektra | B8 V |
Paralaksi (mas) | 17.62 |
Umbali (miakanuru) | 185 |
Mwangaza halisi | -1.16 |
Masi M☉ | 3.5 |
Nusukipenyo R☉ | 4.9 |
Mng’aro L☉ | 130 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 12300 |
Majina mbadala | Lanx Borealis, β Lib, 27 Librae, BD-08° 3935, FK5 564, HD 135742, HIP 74785, HR 5685, NSV 7009, SAO 140430 |
Zubani Shimali ilijulikana na mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hilo kutoka kwa Waarabu wanaotumia neno الزبان الشمالي al-zuban ash-shamali kwa maana ya « koleo la Kaskazini » yaani koleo la nge. Maana yake nyota hii pamoja nyingine za Mizani zilihesabiwa zamani kuwa sehemu ya Akarabu (Nge) na kutazamiwa kama makoleo yake. Hivyo kundinyota lote la Mizani bado liliitwa “Χηλαι” (helai - makoleo) na Klaudio Ptolemaio katika Almagesti. Kwa nyota aliita “ile angavu kwenye ncha ya koleo la kaskazini”[2].
Kwa matumizi ya kimataifa UKIA ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota ya Lib β kwa tahajia ya "Zubeneschamali" [3].
Beta Librae ni jina la Bayer; Beta ni herufi ya pili katika Betabeti ya Kigiriki lakini Zubani Shimali ni nyota angavu zaidi na hii ni mfano ya kwamba Bayer hakufuata mwangaza kamili wakati wa kuorodhesha nyota.
α Beta Librae iko kwa umbali wa miakanuru 185 kutoka Jua letu. Vipimo vya spektra vinaonyesha ya kwamba iko mwanzoni kwenye safu kuu ya nyota ikipangwa katika kundi la spektra B8. Maana yake ina jotoridi kubwa, inang‘aa sana na kubiringia haraka kwenye mhimili wa mzunguko wake.
Iko katika mchakato wa kuyeyunganisha hidrojeni yake kuwa heli. Kwa kawaida nyota za aina hii zinaonekana nyeupe au buluu kutokana na jotoridi kubwa usoni lakini Zubani Shimali inaonekana kwa rangi ya kijani kwa watazamaji wengi. Ni nyota ya pekee inayoonekana hivyo kwa watu wengine lakini si watazamaji wote wanaokubali.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.