From Wikipedia, the free encyclopedia
Zubani Junubi (kwa Kilatini na Kiingereza Zubenelgenubi; pia α Alfa Librae, kifupi Alfa Lib, α Lib) ni kati ya nyota angavu katika kundinyota la Mizani (Libra).
(Alfa Librae, Zubenelgenubi) | |
---|---|
Kundinyota | Mizani (Libra) |
Mwangaza unaonekana | α1 5.15 'α2': .2.74 – |
Kundi la spektra | α1 F3 V |
Paralaksi (mas) | α1: 43.52 ± 0.43 α2 : 43.03 ± 0.19 |
Umbali (miakanuru) | α1: 74.9 α2 : 75.8 |
Mwangaza halisi | α1: +3.35 α2 : +0.92 |
Masi M☉ | α1: 2 α2: 1.5 |
Nusukipenyo R☉ | α1 : 1.48 α2: 2.78 |
Mng’aro L☉ | α1: 3.9 α2 : 36 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | α1: 6770 α2 : 8730 |
Majina mbadala | α1 Lib: 8 Librae, BD–15 3965, FK5 1387, HD 130819, HIP 72603, HR 5530, SAO 158836. α2 Lib: 9 Librae, BD–15 3966, FK5 548, HD 130841, HIP 72622, HR 5531, SAO 158840 |
Zubani Junubi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaotumia neno الجنوبي الزبان al-zuban al-janubi kwa maana ya « koleo la kusini » yaani koleo la nge. Maana yake nyota hii pamoja na nyingine za Mizani zilihesabiwa zamani kuwa sehemu ya Akarabu (Nge) na kutazamwa kama makoleo yake. Hivyo kundinyota lote la Mizani bado liliitwa “Χηλαι” (helai - makoleo) na Klaudio Ptolemaio katika Almagesti. Kwa nyota aliita “ile angavu kwenye ncha ya koleo la kusini”[2].
Kwa matumizi ya kimataifa UKIA ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota ya Lib α² kwa tahajia ya "Zubenelgenubi" [3]. Maana Zubani Junubi ni nyota maradufu na azimio la Ukia linahusu nyota kuu katika mfumo huu.
Alfa Librae ni jina la Bayer; Alfa ni herufi ya kwanza katika alfabeti ya Kigiriki lakini Zubani Junubi ni nyota angavu ya pili na hii ni mfano ya kwamba Bayer hakufuata mwangaza kamili wakati wa kuorodhesha nyota.
α alfa Librae iko kwa umbali wa miakanuru 77 kutoka Jua letu. Ni nyota maradufu inayoonekana kwa darubini kuwa na nyota mbili ndani yake zinazoitwa α1 Librae na α2 Librae. α2 ni nyota angavu zaidi na umbali kati ya sehemu hizi mbili ni vizio astronomia 5.400. Vipimo vya spektra vinaonyesha ya kwamba kila moja ni nyota maradufu tena kwa hiyo Zubani Junubi ni mfumo wa angalau nyota nne zinazozungukana kwa namna ya jozi mbili za nyota.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.