Justin mfiadini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Justin mfiadini

Justin (pia Yustino Shahidi; Kiing. Justin Martyr; alizaliwa Flavia Neapolis, leo Nablus, Palestina, 103 hivi - Roma, Italia, kati ya 162 na 168) alikuwa mwanafalsafa ambaye, kisha kuongokea hekima halisi katika ukweli wa Yesu, aliishika katika mwenendo wa maisha yake, aliifundisha chuoni, akieneza na kutetea Ukristo hata kwa maandishi maarufu, na hatimaye akakamilisha ushahidi wake kwa kuuawa katika dhuluma ya kaisari Marko Aureli wa Dola la Roma.

Thumb
Picha takatifu ya Kirusi ya Mt. Justin.

Ni kwamba, baada ya kumpatia kaisari huyo utetezi wa Wakristo, alitolewa kwa mtawala Rusticus akakiri imani mbele yake na kwa ajili hiyo aliuawa pamoja na wanafunzi wake sita (Karitoni, Karito, Evelpisto, Gerasi, Peoni na Liberiani) [1].

Hati za mateso yao zimetunzwa hadi leo[2].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Walutheri na Waanglikana kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Juni[3].

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.