Yohane Mvunaji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Mvunaji (kwa Kiitalia: Giovanni Theristis; Palermo, mkoa wa Sicilia, Italia, 1049 – Stilo, Calabria, 1129) alikuwa mmonaki wa Ukristo wa Mashariki katika mkoa asili ya wazazi wake, Calabria[1].
Aliitwa "Mvunaji" kwa sababu ya huruma yake kwa maskini iliyomfanya aende mara nyingi kuwasaidia shambani[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi sawia kama mtakatifu, ingawa aliishi baada ya farakano kati yao.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Februari[3].
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.