Milima ya Ghat ya Magharibi ni eneo la milima inayoenea katika urefu wa km 1,600 sambamba na pwani ya magharibi ya Bara Hindi, kupitia majimbo ya Kerala, Tamil Nadu, Karnataka, Goa, Maharashtra na Gujarat[1].
Ni eneo lililoandikishwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia likiwa kati ya vitovu vya bioanwai[2]. Kuna idadi kubwa ya spishi za wanyama na mimea ambayo inapatikana nchini Uhindi pekee.
Jina
Jina la "ghat" katika lugha za Kihindi linamaanisha "safu ya milima". Safu hiyo ina athira kubwa kwa hali ya hewa na mwendo wa masika ya monsuni (pepo za msimu katika Bahari Hindi) yanayoonyesha kwa wingi kwenye mitelemko ya magharibi ya Ghat ilhali kiasi kinachofika upande wa mashariki ni kidogo.
Maeneo
Masafa ya milima ya Ghat huanzia kaskazini kuelekea kusini kando ya magharibi na kuacha tambarare nyembamba kwenye pwani ya magharibi.
Maeneo mengi ndani ya Ghat yametengwa kama hifadhi ya taifa au misitu inayohifadhiwa. [3]
Masafa huanza karibu na mji wa Songadh wa Gujarat, na kuishia karibu na ncha ya kusini ya Uhindi. Eneo la milima hii lina jumla ya kilomita za mraba 160,000 na kuwa eneo la kukusanya maji kwa mito inayomwagilia asilimia 40 za Uhindi. Mwinuko wa wastani ni mnamo mita 1,200 juu ya UB. [4]
Vilele
Ghat ya Magharibi huwa na milima mirefu inayofikia kimo cha zaidi ya mita 2000. Mlima Anamudi (mita 2,695) ndio mlima mrefu zaidi.
Chanzo cha mito
Mvua inayonyesha kwenye Ghat ya Magharibi unalisha mito mingi ya kudumu ya Uhindi. Mifumo mikubwa ya mito inayotokea kwenye Ghat ya Magharibi, hii ni pamoja na mito ya Godavari, Kaveri, Krishna, Thamiraparani na Tungabhadra . Mito mingi midogo zaidi yenye chanzo kwenye Ghat inajiunga na mito hiyo, na hubeba maji mengi wakati wa miezi ya masika. Mito hiyo inaelekea hasa upande wa mashariki ikifuata mtelemko wa nchi ikiishia kwenye Ghuba ya Bengali.
Mito ya Periyar, Bharathappuzha, Pamba, Netravati, Sharavathi, Mandovi na Zuari inashuka upande wa magharibi ikiishia katika Bahari Arabu. Kutokana na mtelemko mkali upande huu inashuka kwa kasi kali.
Mvua
Kanda ya Maharashtra kwa wastani hupata mvua nzito kuliko mikoa ya Karnataka, Kerala na Goa. Katika Maharashtra mvua inaenea sawasawa zaidi kwa sababu mabonde mengi yanaruhusu sehemu za mawingu kupita safu ya Ghat. Lakini Ghat huko Karnataka inaacha nafasi chache za mawingu kupita hivyo miteremko ya magharibi ya Karnataka hupokea mvua kubwa, zaidi ya sm 400, kushinda sehemu nyingine za Ghat ya Magharibi.
Mahali | Eneo | Kiwango cha mvua cha mwaka (milimita)[5] |
---|---|---|
Agumbe | Thirthahalli, Karnataka | mm 7624 |
Amboli | Sindhudurg district, Maharashtra | mm 3859 |
Hulikal | Hosanagara, Karnataka | 5316 |
Amagaon | Khanapur, Karnataka | mm 4089 |
Kakkalli | Sirsi, Uttara Kannada district, Karnataka | mm 4921 |
Nilkund | Sirsi, Uttara Kannada district, Karnataka | mm 4369 |
Mahabaleshwar | Satara district, Maharashtra | mm 5761 |
Devimane | Sirsi, Uttara Kannada district, Karnataka | mm 3981 |
Surli | Hosanagara, Karnataka | mm 4335 |
Lonavla | Pune district, Maharashtra | mm 4073 |
Charmadi | Mudigere, Karnataka | mm 4131 |
Samse | Mudigere, Karnataka | mm 3914 |
Kollur | Udupi district, Karnataka | mm 4992 |
Makkiyad | Wayanad district, Kerala | mm 3714 |
Kudremukh | Chikmagalur district, Karnataka | mm 4158 |
Rajamalai | Idukki, Kerala | mm 4785 |
Nyamakad | Idukki, Kerala | mm 3007 |
Sholayar | Coimbatore, Tamil Nadu | mm 3024 |
Vythiri | Wayanad district, Kerala | mm 4000 |
Pookode | Wayanad district, Kerala | mm 3957 |
Dhamanohol | Mulshi taluka, Maharashtra | mm 6255 |
Mulshi | Pune district, Maharashtra | mm 5100 |
Tamhini Ghat | Mulshi taluka, Maharashtra | mm 5255 |
Chinnakallar | Coimbatore, Tamil Nadu | mm 2947 |
Rock Rock | Uttara Kannada district, Karnataka | mm 5132 |
Mamalia
- Gats Magharibi ina idadi kubwa zaidi ya tiger nje ya Sunderbans .
- Macaque iliyokuwa hatarini iliyo na hatarishi ni hatari kwa Gats Magharibi.
- Kanda ya Magharibi ya Ghats ina idadi kubwa zaidi ya ndovu ya India nchini India.
- Ni watu 100 tu wa Nilgiri tahr waliachwa mnamo 2001 lakini walipatikana kufikia 3,300 kufikia 2010.
- Nilgiri langur ya mwisho iko hatarini.
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.