From Wikipedia, the free encyclopedia
Watitani (kutoka Kigiriki: Τiτᾶνες , titânes - "wanaojikazia") walikuwa nasaba ya pili ya miungu katika mitholojia ya Kigiriki. Jina hilo linataja idadi ya miungu 12 ambao, katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale, walikuwa watoto wa Gaia na Uranos.
Katika imani ya Wagiriki wa Kale walitawala ulimwengu kabla ya nasaba ya miungu wa Olimpos, ambao walipigania udhibiti wa ulimwengu katika mfululizo wa vita kadhaa unaojulikana kama vita ya Watitani (titanomachy). Waolimpo walishinda na Waitani wengi walifukuzwa mbinguni na kufungwa katika vilindi vya Tartaro.
Kizazi cha kwanza cha Watitani walikuwa wana wa Gaia na Uranos wanaoitwa pia Watitani wazee; walikuwa kumi na wawili kwa jumla.
Kizazi cha pili cha Watitani walikuwa watoto wa wale kumi na wawili wa asili. Hao ni pamoja na watoto wa Okeanos na Tethys: potamoi waliotazamwa kama miungu ya mito, na Okeanidi, ambao walikuwa pepo wa bahari elfu tatu kwa idadi, na vilevile Nephelai, waliokuwa mapepo ya mawingu.
Basi kulikuwa na uzao wa Koios na Phoebe: dada Asteria na Leto .
Baadaye walikuja watoto ambao Hyperion alizaa na Theia : Helios (Jua), Selene (Mwezi), Eos (Alfajiri).
Baadaye wakaja wana wa Iapetos na Okeanidi Asia / Klymene:Atlas (mkubwa), Prometheus na Epimetheus (ambao walikuwa mapacha), na Menoitios .
Mwishowe watoto wa Krios na Eurybia (binti wa Gaia na Pontu ) walikuwa wa mwisho: Pallas, Astraeus, na Perses. Perses angeendelea kumwoa Asteria akizaa naye Hekate, mungu wa uchawi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.