From Wikipedia, the free encyclopedia
Wafiadini wa China ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali waliouawa kwa ajili ya imani yao huko China miaka 1648–1930.
Wengi walikuwa wananchi, hasa walei; wengine walikuwa wamisionari kutoka nchi mbalimbali, wakiwemo maaskofu, mapadri, mabruda na masista.
Kanisa la Kiorthodoksi linatambua kama watakatifu wafiadini waumini wake 222 waliouawa wakati wa Uasi wa Waboksa wa mwaka 1900. Wa kwanza kati yao ni Metrophanes, Chi Sung.
Kanisa Katoliki linatambua vilevile waumini 120 ambao waliuawa katika miaka 1648-1930 wakatangazwa watakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000. Wa kwanza wao alikuwa mmisionari Fransisko Ferdinando de Capillas, lakini anayetajwa zaidi ni padri Mchina Augustino Zhao Rong. Kati yao, 87 walikuwa Wachina walei na 33 walikuwa wamisionari kutoka nje; 86 waliuawa katika Uasi wa Waboksa.
Waprotestanti wengi pia waliuawa, lakini hakuna orodha yao rasmi, wala utaratibu wa kuwapa heshima ya pekee.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.