From Wikipedia, the free encyclopedia
Visensya Gerosa (kwa Kiitalia Vincenza Gerosa; (29 Oktoba 1784 – 20 Juni 1847) alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, pamoja na Bartolomea Capitanio, alianzisha shirika la Masista wa Upendo wa Lovere, ambao kwa kawaida wanaitwa Masista wa mtoto Maria[1].
Visensya alizaliwa katika kijiji cha Lovere, mkoani Lombardia, katika familia tajiri. Jina lake la awali lilikuwa Caterina.
Alikutana na Bartolomea alipokuwa na umri wa miaka 40, wakaungana kupambana na ujinga na ufukara wa watu wa eneo lao.
Baada ya Bartolomea kufariki, Visensya aliendeleza shirika lao kwa miaka mingi akafariki mwaka 1847 hukohuko Lovere.
Wote wawili walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 30 Mei 1926, halafu watakatifu na Papa Pius XII tarehe 18 Mei 1950.
Sikukuu ya Visensya inaadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Juni[2].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.