Vanga (kutoka Kimalagasi: vanga) ni ndege wa familia Vangidae. Wanatokea Madagaska tu isipokuwa vanga buluu wa Komori ambaye anatokea kisiwa cha Mwali katika Komori. Takriban spishi zote zina rangi ya nyeusi, kijivu au kahawa juu na nyeupe au pinki chini, lakini chache zina rangi ya buluu na vanga domo-buluu ni mweusi mwenye mgongo mwekundu na vanga wa Bernier ni mweusi kabisa (jike ana rangi ya kahawa). Ndege hawa wana sauti ya filimbi. Hula wadudu, nyungunyungu, mijusi na amfibia, pengine matunda pia. Hulijenga tago lao kwa vijiti, chamba cha mti, mizizi na majani mtini. Jike huyataga mayai 2-4.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Vanga |
Vanga kichwa-cheupe |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
Familia ya juu: |
Corvoidea (Ndege kama kunguru)
|
Familia: |
Vangidae (Ndege walio na mnasaba na vanga)
|
|
Ngazi za chini |
Jenasi 15:
- Artamella W.L. Sclater, 1924
- Calicalicus Bonaparte, 1854
- Cyanolanius Bonaparte, 1854
- Euryceros Lesson, 1831
- Falculea I. Geoffroy Saint-Hilaire, 1836
- Hypositta A. Newton, 1881
- Leptopterus Bonaparte, 1854
- Mystacornis Sharpe, 1870
- Newtonia Schlegel & Pollen, 1868
- Oriolia I. Geoffroy Saint-Hilaire, 1838
- Pseudobias Sharpe, 1870
- Schetba Lesson, 1831
- Tylas Hartlaub, 1862
- Vanga Vieillot, 1816
- Xenopirostris Bonaparte, 1850
|
Funga
- Artamella viridis, Vanga Kichwa-cheupe (White-headed Vanga)
- Calicalicus madagascariensis, Vanga Mkia-mwekundu (Red-tailed Vanga)
- Calicalicus rufocarpalis, Vanga Mabega-mekundu (Red-shouldered Vanga)
- Cyanolanius madagascarinus, Vanga Buluu (Blue Vanga)
- Cyanolanius m. comorensis, Vanga Buluu wa Komori (Comoro Blue Vanga)
- Euryceros prevostii, Vanga Domo-buluu (Helmet Vanga)
- Falculea palliata, Vanga Domo-mundu (Sickle-billed Vanga)
- Hypositta corallirostris, Vanga Domo-jekundu (Nuthatch Vanga or Coral-billed Nuthatch-vanga)
- Hypositta perdita, Vanga wa Bluntschli (Bluntschli's Vanga or Short-toed Nuthatch-vanga) - taxonomic status questionable
- Leptopterus chabert, Vanga Macho-buluu (Chabert's Vanga)
- Mystacornis crossleyi, Vanga wa Crossley (Crossley's Vanga)
- Newtonia amphichroa, Vanga Mgongo-kijivu (Dark Newtonia)
- Newtonia archboldi, Vanga wa Archbold (Archbold's Newtonia)
- Newtonia brunneicauda, Vanga Mkia-kahawia (Common Newtonia)
- Newtonia fanovanae, Vanga Kichwa-kijivu (Red-tailed Newtonia)
- Oriolia bernieri, Vanga wa Bernier (Bernier's Vanga)
- Pseudobias wardi, Vanga Shore (Ward's Flycatcher)
- Schetba rufa, Vanga Mgongo-mwekundu (Rufous Vanga)
- Tylas eduardi, Vanga Kichwa-cheusi (Tylas Vanga)
- Vanga curvirostris, Vanga Domo-kulabu (Hook-billed Vanga)
- Xenopirostris damii, Vanga wa Van Dam (Van Dam's Vanga)
- Xenopirostris polleni, Vanga wa Pollen (Pollen's Vanga)
- Xenopirostris xenopirostris, Vanga wa Lafresnaye (Lafresnaye's Vanga)
Vanga macho-buluu
Vanga domo-kulabu
Vanga wa Lafresnaye
|
Makala hii kuhusu "Vanga" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili vanga kutoka lugha ya Kimalagasi. Neno (au maneno) la jaribio ni vanga. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.
|