Kipanya wa Rudd (Uranomys ruddi) ni mnyama mgugunaji mdogo na spishi pekee ya jenasi Uranomys wa nusufamilia Deomyinae katika familia Muridae aliye na nasaba karibu na vipanya manyoya-magumu.
Kipanya wa Rudd | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanya wa Rudd | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Maelezo
Kipanya huo ana ukubwa zaidi kuliko vipanya wa kawaida. Urefo wa mwili ni sm 8.4-13.4 na urefu wa mkia ni sm 5.3-7.9. Uzito ni g 41-53. Manyoya kwenye mgongo ni magumu kama yale ya vipanya manyoya-magumu lakini siyo kama yale ya vipanya-miiba. Upande wa juu na mbavu zina rangi ya kahawa na upande wa chini ni mweupe. Miguu imefunikwa kwa manyoya meupe.
Kipanya wa Rudd hujulikana kupitia msambao mkubwa katika Afrika kusini kwa Sahara, pamoja na angalau Kenya, Tanzania na Uganda katika Afrika ya Mashariki, lakini kamwe wako wengi. Kwa kawaida hukamatwa katika makazi ya savana. Anafikiriwa kukiakia usiku na hula wadudu hasa.
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.