From Wikipedia, the free encyclopedia
Urani (kwa Kiingereza uranium) ni elementi katika mfumo radidia yenye alama U. Namba atomia ni 92 na uzani atomia ni 238. Atomi yake ina protoni 92 na elektroni 92.
Urani (uranium) | |
---|---|
Mtapo wa urani | |
Jina la Elementi | Urani (uranium) |
Alama | U |
Namba atomia | 92 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 238.0289 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 21, 9, 2 |
Densiti | 19.1 g·cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 1405.3 K (1132.2 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4404 K (4131 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 3 · 10-4 % |
Hali maada | mango |
Jina limechaguliwa kutokana na sayari iliyoitwa Uranus kwa kumbukumbu ya mungu mmojawapo wa Dola la Roma.
Urani ni metali nururishi. Isotopi za kawaida katika urani ni urani-238 na urani-235.
Urani ina uzani atomia wa juu kati ya elementi zote zinazotokea kiasili maana yake masi ya atomu yake ni kubwa zaidi. Hata hivyo densiti yake si juu zaidi hivyo mchemraba wa cm³ 1 wa urani ni mwepesi kuliko mchemraba wa cm³ 1 wa dhahabu.
Urani ni metali nyeupe nururishi katika mfululizo wa aktinidi. Isotopi yake 235U ni dutu asilia pekee inayoweza kuwa na mmenyuko mfululizo wa kinyuklia.
Kwa sababu hiyo hutumiwa katika tanuri nyuklia na katika silaha za nyuklia kwa ajili ya vita. Bomu la nyuklia la kwanza lililorushwa juu ya Hiroshima lilitengenezwa kwa urani.
Ikiwa ni metali nururishi pekee inayopatikana duniani kiasili hutumiwa kwa utengenezaji wa umeme katika tanuri nyuklia. Takriban asilimia 10 ya umeme duniani hutengenezwa kwa njia hii, katika nchi kadhaa ni sehemu kubwa ya umeme[1].
Mwanzoni mwa upatikanaji wa teknolojia hiyo katika karne ya 20 kulikuwa na matumaini makubwa ya kuwa italeta umeme nafuu kwa watu wote hasa tangu ilitambuliwa ya kwamba akiba za makaa mawe na mafuta ya petroli zitakwisha. Ila tu matatizo ya takataka nyuklia na ajali hatari za tanuri nyuklia yalichelewesha maendeleo ya matumizi yake. Vilevile maendeleo ya uzalishaji wa nishati mbadala kama vile umemejua au umeme wa upepo yalileta mitazamo mipya.
Tena upatikanaji wa urani yenyewe ni tatizo kwa sababu akiba za urani duniani zinazofaa kwa uchimbaji rahisi kiuchumi hukadiriwa kudumu kwa miaka 50-100 pekee.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.