From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Ukerewe ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Mwanza.
Eneo la wilaya hiyo liko kwenye visiwa vya ziwa Viktoria Nyanza, hasa visiwa viwili vikubwa vya Ukerewe na Ukara pamoja na visiwa vidogo kama vile Kweru, Goziba, Sizu, Irugwa, Kerebe na vingine vingi.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 261,944 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 387,815 [2].
Wilaya ya Ukerewe ina makabila makuu matatu ambayo ni Wakerewe, Wakara na Wajita. Kabila kuu zaidi ni la Wakerewe ambalo ndilo jina la kisiwa kikuu pia. Wakara wanapatikana nje kidogo ya kisiwa hicho katika kisiwa cha Ukara. Halafu kuna Wajita ambao asili yao ni mkoa wa Mara.
Ukerewe umewahi kutoa viongozi wakubwa serikalini kama Pius Msekwa, spika wa bunge mstaafu, Gertrude Mongella na wengine wengi. Pia uliwahi kutoa padri wa kwanza mzawa wa Kanisa Katoliki aliyeitwa padri Chipanda lakini pia ni eneo lililojengwa ghorofa la kwanza na mtu Mweusi.
Usafiri ni wa aina kuu mbili: usafiri wa majini na wa ardhini ambao huwarahisishia wakazi wa eneo hili kufanya kazi na shughuli mbalimbali za maendeleo katika wilaya yao.
Ukerewe unasifika kwa kutoa matunda aina ya machungwa ambayo wananchi wake huyatumia kula na kama biashara ili kujiongezea kipato.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.