From Wikipedia, the free encyclopedia
Udadisi (kwa Kiingereza: "curiosity", kutoka neno la Kilatini "curiositas", yaani "umakini") ni tabia ya kuchunguza kitu au jambo kwa kina[1][2].
Mara nyingi wanasayansi ndio wadadisi wazuri kwa maana wao huchunguza kwa kina na umakini, wakifuata kanuni na kutafuta ushahidi. Kwa njia yao udadisi umestawisha maisha ya binadamu[3].
Katika udadisi kuna ule wa kawaida na mwingine usio wa kawaida. Kwa udadisi wa kawaida mtu hudadisi kwa njia rahisi, tofauti na ule usio wa kawaida ambapo mtu asipokuwa makini anaweza hata kufa. Udadisi huu unahitaji kuwa makini sana.
Udadisi unajitokeza mapema katika mtoto[4], lakini unapozidi na kuelekea mambo yasiyo na maana (kwa mfano umbeya) unamzuia mtu asijue mambo ya maana; hapo ni kilema cha akili.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.