From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020 ulifanyika tarehe 28 Oktoba. Wapiga kura walimchagua Rais, wabunge na Madiwani.[1]
| |||||||||||||||||||
| |||||||||||||||||||
|
Kufuatana na tangazo la Tume la Uchaguzi la 30 Oktoba matokeo yalikuwa kama yafuatayo[2]:
Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 29,754,699. Waliopiga kura walikuwa 15,091,950 (% 50.72), wasiopiga kura walikuwa 14,662,749 (% 49.28).
Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 15,091,950. Kura 261,755 ziliharibika. Jumla ya kura halali ilikuwa 14,830,195.
Mgombea | Mgombea Mwenza | Chama | |
---|---|---|---|
Bernard Kamillius Membe | Omar Fakih Hamad [3] | Alliance for Change and Transparency (ACT) | |
Tundu Lissu | Salum Mwalimu Juma | Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) | |
Twalib Ibrahim Kadege | Ramadhan Ali Abdallah | United People's Democratic Party (UPDP) | |
Hashim Rungwe Spunda | Mohammed Massoud Rashid | Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) | |
Leopord Lucas Mahona | Khamis Ali Hassan | National Reconstruction Alliance (NRA) | |
John Magufuli | Samia Suluhu | Chama Cha Mapinduzi | |
Queen Cuthbert Sendiga | Khamis Juma Shoka | Alliance for Democratic Change (ADC) | |
Muttamwega Bhatt Mgaywa | Satia Mussa Bebwa | Sauti ya Umma (SAU) | |
Cecilia Augustino Mwanga | Tabu Mussa Juma | Demokrasia Makini | |
Yeremia Kulwa Maganja | Khamis Haji Ambar | National Convention for Construction and Reform Mageuzi (NCCR Mageuzi) | |
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba | Hamida Huweishil Abdalla | Civic United Front (CUF) | |
Philipo John Fumbo | Zaina Juma Khamis | The Democratic Party (DP) | |
Seif Maalim Seif | Rashid Ligania Rai | Alliance for Tanzania Farmers Party (AFP) | |
Khalfan Mohammed Mazrui | Mashavu Alawi Haji | The Union for Multiparty Democracy (UMD) | |
Baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa kumaliza kutangaza matokeo, vyama vikuu vya upinzani viliungana kukataa matokeo hayo na kudai uchaguzi huru na wa haki chini ya tume huru vikataja kasoro nyingi za mchakato mzima wa uchaguzi[4] [5] [6]
Upande wake Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) ulizuia mitandao ya kijamii mbalimbali ili kupunguza mawasiliano hasa kutokana na mauaji yaliyotokea Zanzibar.[5]
Nchi na taasisi mbalimbali zimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu uchaguzi na matokeo yake [7], [8], [9][10].
Tarehe 10 Novemba 2020, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Haki za Binadamu alitoa tamko kuhusu hali tete ya nchi[11] ambalo lilijibiwa mapema na serikali ya Tanzania[12].
Uchaguzi wa 2020 huhesabiwa kuwa ndiyo mbaya kupita yote. Uligubikwa na hila na mbinu chafu. Mbowe alitoa rai yake juu ya uchaguzi huo kwa kusema, ''Kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''[13]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.