From Wikipedia, the free encyclopedia
Tai walanyoka ni ndege mbua wakubwa kiasi wa nususfamilia Circaetinae katika familia Accipitridae. Tai wa Ufilipino ni labda mwana wa nusufamilia hii, kwa sababu chunguzi za ADN zimeonyesha mnasaba wake. Ndege hawa wana makucha marefu ili kukamata uwimbo na domo kubwa lenye ncha kwa kulabu ili kupapura nyama. Uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kabisa na hutambua uwimbo kwa mbali sana. Tai walanyoka hula nyoka hasa (isipokuwa tai pungu) lakini mijusi na mamalia wadogo pia na pengine ndege na wadudu wakubwa. Hujenga tago lao mtini ambola limefichwa vizuri kati ya majani. Jike hulitaga yai moja tu, au pengine mayai mawili.
Tai mlanyoka | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tai mlanyoka kahawia | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.