Simujanja

From Wikipedia, the free encyclopedia

Simujanja

Simujanja ni aina ya rununu ambayo inafanya mambo mengi kuliko simu nyingine ya kawaida.[1] Zinafanya kazi kama tarakilishi, lakini hiki ni chombo kinachobebeka na kidogo cha kutosha katika mkono wa mtumiaji.

Thumb
Simujanja inayotumika kusoma Wikipedia.
Thumb
Simujanja za Samsung.
Thumb
Simu ya kiganjani ya HTC Desire Z, ikiwa na kioo kikubwa cha kugusa ikionesha baobonye ya QWERTY.

Matumizi yake ni pamoja na:

Kwa sababu simujanja ni kama tarakilishi ndogo, zinaweza kuendeshwa kwa kutumia mifumo ya uendeshaji kama vile Apple iOS na Android - itategemea na mahitaji ya chombo chenyewe. Lakini vilevile wengine wanatumia Windows Phone au BlackBerry OS.[2]

Historia

Thumb
IBM Simon (1994)[3]

Simu ya kwanza kuuzwa ambayo inaweza kuitwa simujanja iliitwa "Angler": ilitengenezwa na Frank Canova mwaka 1992 wakati akifanya kazi IBM.[4][5][6]

Toleo lililoimarishwa zaidi liliuzwa mwaka 1994 na kampuni ya BellSouth kwa jina la Simon Personal Communicator. Pamoja na kupia na kupokea simu, simu hii iliweza pia kutuma nukushi na barua pepe. Simu hii ilikuwa na ramani, kalenda, kitabu cha namba za simu, saa, n.k.[7]

Neno "simujanja" halikutumika hadi mwaka mmoja baada ya kutolewa kwa simu hiyo.

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.