Jamhuri ya Shirikisho ni muundo wa kisiasa ambako jamhuri hutazamiwa kama maungano wa maeneo ndani yake -kwa kawaida huitwa "majimbo"- yenye haki zao zisizopewa wala zisizonyanganywa na serikali kuu ya kitaifa.
Katika muundo huu taifa hatawaliwi na serikali moja katika mambo yote lakini madaraka hugawiwa kati ya madaraka ya serikali ya kitaifa na madaraka ya majimbo.
Mara nyingi maazimio kuhusu mambo ya utamaduni hubaki kwenye ngazi ya jimbo lakini pia sehemu za kodi na sisasa ya kiuchumi. Siasa ya nje na mambo ya jeshi hushikwa na serikali kuu. Mambo mengine hutegemea na utaratibu wa kikatiba katika kila nchi.
Mifano ya jamhuri za shirikisho:
- Afrika Kusini
- Argentina
- Austria tangu 1918, tena 1945
- Brazil
- Ethiopia
- Komori
- Marekani tangu 1776
- Meksiko
- Nigeria
- Ujerumani
- Uhindi tangu 1947
- Urusi
- Uswisi tangu 1848
Si lazima ya kwamba kila shirikisho ni jamhuri. Mifano ya falme ya shirikisho ni Falme za Kiarabu na Malaysia; kihistoria pia Dola la Ujerumani hadi 1918.
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.