Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sentensi ni kundi la maneno ambalo lina kiima na kiarifa na hutoa maana kamili; ndiyo kipashio cha juu kabisa katika tungo.
Kuna aina kuu nne za sentensi nazo ni:
1. Sentensi sahili - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa kishazi huru kimoja tu, mfanoː Mama anakula.
2. Sentensi changamano - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa kishazi tegemezi na kishazi huru, mfanoː Mtoto aliyepotea ameonekana.
3.Sentensi ambatano - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa sentensi mbili zilizounganishwa na kiunganishi, mfanoː Baba analima ingawa mama anakula.
Sentensi ambatano huweza kuundwa kwaː a. sentensi sahili + sentensi sahili. b. Sentensi sahili + sentensi changamano. c. Sentensi changamano + sentensi changamano.
4. Sentensi shurutia - Hii ni aina ya sentensi iliyoundwa kwa mofimu za masharti, mfanoː ki, nge, ngeli pamoja na ngali. Njia za uchanganuzi wa sentensiː a. Njia ya matawi au ngowe. b. Njia ya mishale au mistari. c. Njia ya visanduku au jedwali. d. Njia ya maneno.
Hatua za uchanganuzi wa sentensiː 1. Kuainisha sentensi husika 2. Kugawa sentensi katika kiima na kiarifu 3. Kuonesha vipashio vya kiima na kiarifu 4. Kuainisha aina za maneno 5. Kuandika sentnsi husika kwa kila panapohusika
Sentensi huundwa kwa sehemu kuu mbili:
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sentensi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.