From Wikipedia, the free encyclopedia
Satelaiti (pia setelaiti, setilaiti, kutoka Kilatini satelles, "msindikizaji", kupitia Kiingereza satellite) ni kitu kinachofuatana na kitu kingine. Neno linatumiwa kwa maana mbili ambayo ni:
Kwa kufuata maana hii ya 2, Satelaiti au Setilaiti ni kifaa cha kuundwa na binadamu ambacho huundwa kwa kusudi la kukiweka kwenye obiti kwaajili ya shughuli maalumu kama vile utafiti wa kisayansi. Mara nyingine vifaa hivi huitwa satelaiti za kutengenezwa ili kuzitofautisha na satelaiti asilia kama vile mwezi wa Dunia.
Katika astronomia satelaiti ni gimba dogo linalozunguka gimba kubwa zaidi kwa njia ya obiti (en:orbit). Satelaiti ni hasa gimba linalozunguka sayari; kwa maana hii ni sawa na "mwezi" lakini inatumiwa pia kwa galaksi ndogo inayozunguka galaksi kubwa zaidi. Kuna pia asteroidi zenye satelaiti zao.
Kila satelaiti inashikwa na graviti ya gimba kubwa zaidi, kama ni sayari au asteroidi au galaksi.
Dunia inazungukwa na maelfu ya satelaiti ambazo ni vifaa au vyombo vilivyorushwa katika anga-nje kwa njia ya roketi na kuzunguka Dunia kwa obiti mbalimbali. Satelaiti hizi zinatekeleza kazi za kisayansi, za kibiashara na za kijeshi.
Satelaiti ya kwanza iliyorushwa angani ilikuwa Sputnik 1. Ilitumwa na Umoja wa Kisovyeti tarehe 4 Oktoba 1957.
Siku hizi kuna nchi zaidi ya 50 zilizopeleka satelaiti katika anga-nje. Idadi za nchi zenye uwezo wa kuzirusha ni ndogo zaidi.
Tangu Sputnik 1 takriban satelaiti 6,600 zimepelekwa angani. Mwaka 2013 ilikadiriwa ya kwamba 3,600 bado zilifuata obiti zake. [1] Takriban 1,000 zilifanya kazi;[2] lakini nyingine hazikufanya kazi tena, zilikuwa takataka ya angani.
Takriban satelaiti 500 ziko kwenye obiti za dunia (chini ya kilomita 2,000 juu ya uso wa Dunia), 50 ziko kwenye obiti ya wastani (mnamo 20,000 km) ambazo hasa zile za uongozaji na nyingine ziko kwenye obiti ya juu ambako zinaweza kukaa muda wote juu ya eneo lilelile la Dunia (mnamo 36,000 km).[3]
Vyomboanga vya utafiti vilipelekwa hadi obiti za kuzunguka sayari mbalimbali na sasa zimekuwa satelaiti za sayari hizo kama vile Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii, Zohali, asteroidi kadhaa[4] na pia Jua.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.