ukarasa wa maana wa Wikimedia From Wikipedia, the free encyclopedia
Roma (pia: Rumi) ni jina linalotumika kwa mji wa Roma (mji mkuu wa Italia), ama kwa dola la Roma lililokuwa kwa karne kadhaa kabla na baada ya Kristo dola kubwa kuliko zote duniani, tena kwa Kanisa la Roma ambalo ni kiini cha Kanisa Katoliki lote. Lilikuwa pia jina la mungu wa kike katika dini ya Roma ya Kale.
Roma ni umbo asili la jina katika Kilatini na Kiitalia; limekuwa pia la kawaida katika Kiswahili cha kisasa.
Kumbe "Rumi" ilikuwa kawaida katika Kiswahili cha zamani kutokana na kawaida ya lugha ya Kiarabu (الرُّومُ ar-Rūm).
Matoleo ya Biblia ya "Union Version" iliyochapishwa tangu 1952 hutumia "Rumi", "Warumi". Kumbe tafsiri ya Biblia ya "Kiswahili cha Kisasa" hutumia "Roma", "Waroma".
21 Aprili 753 KK ndiyo tarehe ya kimapokeo ambayo mji huo ulisemekana kuundwa na mapacha Romulo na Remo. Ukweli ni kwamba ulianzishwa mapema zaidi (1000 K.K. hivi).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.