From Wikipedia, the free encyclopedia
Robert Fisk (12 Julai 1946 – 30 Oktoba 2020) alikuwa mwandishi na mwanahabari raia wa Uingereza na Eire. Aliandika hasa kuhusu hali ya nchi za Mashariki ya Kati kuanzia mwaka 1976 hadi kifo chake.
Kuanzia 1989 hadi kifo chake, alikuwa mwandishi wa Independent. [1] Fisk alizaliwa Maidstone, Kent .
Fisk alisoma katika Chuo Kikuu cha Lancaster na katika Chuo cha Trinity Dublin.
Alijua vizuri sana lugha ya Kiarabu[2]. Alikuwa mmoja wa wanahabari wachache waliopata nafasi ya kumhoji Osama bin Laden. Alimhoji mara tatu kati ya miaka 1993 na 1997. [3]
Fisk alifariki kwa kiharusi mnamo 30 Oktoba 2020 katika hospitali ya Dublin, Ireland akiwa na umri wa miaka 74. [4]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.