From Wikipedia, the free encyclopedia
Nzi-gome (kutoka Kiing.: barkfly) ni wadudu wadogo (mm 1-10) wa oda Psocodea (psokhos = iliyotafunwa, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Spishi zinazoishi ndani ya majengo huitwa chawa-vitabu. Zamani spishi fulani za nusuoda Troctomorpha ziligeuka kuwa chawa vidusia. Kwa hivyo siku hizi wataalamu wanaweka chawa katika Psocodea kama oda ndogo Phthiraptera chini ya Troctomorpha.
Nzi-gome | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Metylophorus nebulosus | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusuoda 3:
| ||||||||||||
Wadudu hawa wana mwili kwa muundo wa msingi. Paji ya kichwa imefura, macho ni makubwa kwa kulinganisha na wana oseli tatu. Mandibuli ni kwa kutafuna na ndewe ya kati ya maxila imegeuka katika kifito ambacho kinakaza mdudu akiparua mboji. Wakiwa na mabawa, haya huwekwa kama hema. Pengine urefu wa yale ya mbele ni 50% zaidi ya yale ya nyuyma.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nzi-gome kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.