From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuhusu matumizi ya jina "Utaridi" kwa sayari hii tazama chini kwa "jina"
134340 Pluto | |
---|---|
Pluto, New Horizons mnamo Julai 2015. | |
Ugunduzi | |
Mgunduzi | Clyde W. Tombaugh |
Tarehe | 18 Februari 1930 |
Jina | |
Asili ya jina | Kla. Plūtō, kutokana na Kgk. Πλούτων (Ploutōn) |
Alama | na |
Tabia za mzunguko | |
Mkaribio | km 4,436,820,000 au 29.658 |
Upeo | km 7,375,930,000 au 49.305 |
km 5,906,380,000 au 39.482 | |
Uduaradufu | 0.2488 |
siku 90,560 miaka 247.94 | |
Mwinamo | 17.16° |
Miezi | 5 |
Tabia za maumbile | |
km 1,188.3±0.8 mara 0.1868 ya Dunia mara 0.684 ya Mwezi | |
Tungamo | kg (1.303±0.003)×1022 mara 0.00218 ya Dunia mara 0.177 ya Mwezi |
g/cm3 1.854 | |
Uvutano wa usoni | m/s2 0.620 |
Kasi ya kuponyokea | km/s 21.3 |
siku −6.38680 | |
siku −6.387230 | |
Weupe | 0.72 (Bond) 0.52 (jiometri) |
Halijoto | K 44 (−229°C) |
Pluto (alama: [1] au [2]) ni sayari kibete inayozunguka jua ng'ambo ya obiti ya Neptuni.
Masi yake ni hasa mwamba na barafu. Kipenyo chake ni km 2,390.
Katika mwendo wake inakata njia ya Neptune kwa sababu njia yake ina umbo la duaradufu kali.
Pluto ina miezi mitano inayoitwa Charon, Styx, Nix, Kerberos na Hydra. Charon ni kama nusu ya ukubwa wa Pluto (kipenyo km 1200) na umbali wa wastani ni km 19,410. Styx, Nix, Kerberos na Hydra ni miezi midogo (vipenyo: km 10-25, 56x26, 31 na 43x33) yenye umbali wa km 42,600, 48,600, 57,700 na 64,700 kutoka Pluto.
Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari ya tisa katika mfumo wa Jua toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006. Vipimo vipya vilileta wasiwasi juu ya swali: Je, sayari ni kitu gani?, hasa baada ya kugundua magimba ya ziada nje ya Pluto yanayokaribia ukubwa wake lakini hayafai kuitwa sayari.
Umoja wa kimataifa wa wanaastronomia uliondoa Pluto katika orodha ya sayari kwenye mkutano wake wa mwaka wa 2006. Badala yake wameiita sayari kibete. Hata hivyo baadhi ya wanaastronomia walipinga uamuzi huu.
Jina "Pluto" linamtaja mungu mtawala wa kuzimu katika mitholojia ya Roma ya Kale. Limechaguliwa kwa sayari hii kutokana na umbali wake na jua na giza kubwa liliko sawa na hali ya giza ambayo ni mfano wa kuzimu.
Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Utaridi[3] [4] [5] kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini mabaharia Waswahili wametumia jina hili la "Utaridi" tangu miaka mingi kwa ajili ya sayari ya kwanza (ing. "Mercury").[6]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.