Petro wa Betancur
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro wa Betancur (Tenerife, Hispania, 21 Machi 1626 - Antigua, Guatemala 25 Aprili 1667), alikuwa mmisionari kutoka Hispania katika Amerika ya Kati.
Alijulikana kama "Mt. Fransisko wa Amerika", naye ni mtakatifu wa kwanza mzaliwa wa funguvisiwa la Kanaria, pia anahesabiwa wa kwanza katika Guatemala na Amerika ya Kati kwa jumla.
Petro alitambulikana kwa unyenyekevu na ugumu wa maisha katika kutekeleza huruma kwa wengine, wakiwemo mayatima, watoto wa mitaani, vijana wasioelimika, ombaomba, wagonjwa,, wageni na waliohukumiwa kufanya kazi za shokoa.[1]
Mwanashirika wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko, alianzisha pia shirika la kwanza la barani Amerika, "Ndugu wa Kiume na wa Kike wa Bethlehemu". Baada ya kufutwa, lilifufuliwa tarehe 16 Januari 1984.
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 22 Juni 1980, halafu mtakatifu tarehe 30 Julai 2002. [1]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.