From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Alexander VI (1 Januari 1431 – 18 Agosti 1503) alikuwa Papa kuanzia tarehe 11/26 Agosti 1492 hadi kifo chake[1]. Alitokea Jativa, Hispania[2].
Alimfuata Papa Innocent VIII akafuatwa na Papa Pius III.
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Roderic Llançol de Borja. Alikuwa Papa wa pili kutoka familia iliyoitwa nchini Italia Borgia. Papa Kalisti III, aliyekuwa wa kwanza, alimsaidia mpwa wake Roderic kupanda ngazi ndani ya Kanisa. Kijana asiyekuwa na mafunzo yoyote wa kiroho, asiyepokea daraja takatifu ya upadri bado, alipewa cheo na mapato ya askofu mara kadhaa katika dayosisi mbalimbali.
Mwaka 1456 alipewa cheo cha kardinali na mwaka 1458 akapadrishwa.
Alizaliana watoto na mke wake wa kando Vannozza dei Cattani akaendelea kuwaangalia na kuwatunza hata alipokuwa Papa. Arusi ya binti yake Lucrezia Borgia ilisheherekewa rasmi katika jumba la Kipapa la Vatikano.
Lakini kabla hajachaguliwa kuwa Papa alimwacha Vannozza akaanza uhusiano na binti Giulia Farnese aliyezaa naye binti mwaka 1492, alipokuwa Papa tayari.
Mwanawe Cesare Borgia alipewa cheo cha askofu alipokuwa na umri wa miaka 16 na cha kardinali alipofikia miaka 18, lakini bila kupewa sakramenti ya daraja takatifu. Baadaye aliacha maisha ya Kanisa akafanywa na baba yake jemadari wa jeshi la Papa.
Aleksanda VI amejulikana pia kwa uamuzi wake wa kugawa dunia kati ya Hispania na Ureno katika mkataba wa Tordesillas mwaka 1494. Mkataba huu ulikuwa msingi wa koloni la Kireno la Brazil na utawala wa Hispania juu ya nchi nyingine za Amerika Kusini na Amerika ya Kati.
Sifa yake nyingine ilikuwa kuhamasisha sanaa za kila aina, kama ilivyokuwa kawaida kwa Mapapa wa Renaissance.
Vilevile alianza urekebisho wa ofisi za Papa.
Wapinzani walimwona kama mfano mbaya wa upotovu wa Upapa wakati wake, wakamsema hata kuliko ukweli wa makosa ambayo aliyafanya na aliyatubu kabla hajafa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.