Niseti wa Trier (pia: Nicetius, Nicetus, Nicet au Nizier; Auvergne[1], leo nchini Ufaransa, 525 hivi - 566 hivi[2]) alikuwa askofu muhimu zaidi wa mji huo[3], leo nchini Ujerumani, akieneza kazi yake hadi Konstantinopoli[4][5][6].

Thumb
Mt. Niseti katika mchoro mdogo.

Gregori wa Tours anamsifu hasa kwa mahubiri yake yenye nguvu, kwa mafundisho yake yenye msimamo na kwa maonyo yake makali [7] yaliyomfanya mfalme Klotari I ampeleke uhamishoni[8].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Oktoba [9].

Tazama pia

Tanbihi

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.