From Wikipedia, the free encyclopedia
Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ambao unatokea akilini, kwa kawaida bila makusudi, katika hatua fulanifulani za usingizi.[1]
Yaliyomo na malengo ya ndoto hayajaeleweka vizuri, ingawa tangu zamani yamejadiliwa sana katika sayansi (hasa elimunafsia) na katika dini. Fani inayochunguza ndoto kisayansi inaitwa onirolojia.[2]
Kwa kiasi kikubwa ndoto zinatokea wakati usingizini macho yanapogeukageuka zaidi, ambapo utendaji wa akili ni mkubwa karibu sawa na mtu anapokuwa macho. Zikitokea wakati mwingine wa usingizi, ndoto hazikumbukwi sana baada ya kuzinduka.[3]
Muda wa ndoto unaweza kuwa tofauti sana: tangu sekunde chache hadi dakika 20–30.[3]
Kwa wastani watu wanapata ndoto 3 hadi 5 kwa usiku, wengine hadi 7[4], lakini nyingi zinasahaulika mara au mapema.[5] Watu wanaweza kukumbuka zaidi ndoto zao wakiamshwa wakati wa huo usingizi wa macho kugeukageuka.
Ndoto zinaelekea kudumu zaidi kadiri muda wa usiku unavyozidi kwenda.[6]
Ndoto zinaweza kuwa za aina mbalimbali: nje ya uwezekano katika maisha ya kawaida, za ajabuajabu, za kutisha, za kusisimua, za kishirikina, za kidini, za kusikitisha, za kijinsia, n.k. Zinaweza pia kumsaidia msanii kubuni kitu.[7]
Kwa kawaida ziko nje ya udhibiti wa mtu, isipokuwa anapoota akiwa anajitambua (ndoto za mchana).[8]
Rai kuhusu maana ya ndoto zimetofautiana sana kadiri ya nyakati na utamaduni.[9]
Kumbukumbu za zamani zaidi kuhusu ndoto ni za miaka 5000 hivi iliyopita huko Mesopotamia, ambapo zilichorwa katika vigae.
Katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale, watu walisadiki ndoto zinaleta ujumbe kutoka kwa mungu fulani au marehemu fulani na kwamba zinatabiri ya kesho.
Wanasayansi wengine wamependekeza kwamba picha nyingi za ndoto zinahusishwa na fahamu. Mwanzoni mwa karne ya 19 na ya 20, nadharia hizo zilijumlishwa na kuendelezwa kwa kiasi kikubwa na Sigmund Freud.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.