From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto Amazonas (kwa Kireno: Rio Amazonas) ndio mto mkubwa kuliko yote duniani. Unabeba maji zaidi kuliko mito ya Nile, Mississippi na Yangtse kwa pamoja.
Chanzo | mlima Nevado Mismi (Peru) |
Mdomo | Atlantiki |
Nchi | Brazil (62.4%), Peru (16.3%) Bolivia (12.0%), Kolombia (6.3%) Ekuador (2.1%) |
Urefu | 6,400 km |
Kimo cha chanzo | takriban 5,597 m |
Tawimito upande wa kulia | Purus, Madeira, Tapajós, Xingu, Tocantins |
Tawimito upande wa kushoto | Marañón, Japurá, Rio Negro |
Mkondo | 219,000 m³/s |
Eneo la beseni | 6,915,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Manaus, Macapa, Santarem |
Una chanzo chake katika milima ya Andes inavuka beseni lake hadi Atlantiki kupitia eneo kubwa la misitu minene. Sehemu kubwa ya mwendo wake iko katika nchi ya Brazil.
Kuhusu urefu hakuna bado mapatano ya kitaalamu kama Nile au Amazonas ndio mto mrefu duniani. Makadirio hutegemea ni tawimto lipi lenye chanzo cha mbali zaidi linaokubaliwa na wataalamu. Mwaka 1969 urefu wake ulipimwa kuwa km 6.400.
Amazonas ina matawimto zaidi ya 10,000 na kati ya hayo 17 yana urefu wa zaidi ya km 1,600 yakishinda mito kama Senegal, Gambia au Nile ya buluu.
Upana wa mto ni wa kilomita kadhaa kufikia hadi 100 wakati wa mafuriko ya kila mwaka. Delta ya Amazonas ina upana wa kilomita mia kadhaa; ndani yake kuna kisiwa cha Marajó chenye eneo la km² 49,000 ambalo ni kubwa kushinda nchi kama Rwanda au Burundi.
Amazonas ni njia muhimu ya mawasiliano na usafiri nchini Brazil. Meli kubwa za baharini zinaweza kuingia hadi bandari ya Manaus iliyoko km 800 ndani ya bara. Meli ndogo za baharini hadi uzito wa tani 3,000 zinaweza kuvuka Brazil yote hadi kufika Peru.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Amazonas (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.