Mswati III wa Uswazi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mswati III wa Uswazi

Mswati III (amezaliwa 19 Aprili 1968[1]) ni mfalme wa Eswatini tangu tarehe 25 Aprili 1986.

Thumb
Mfalme Mswati III mnamo mwaka 2014.
Thumb
Kundi la wake wa Mswati wakikutana na mgeni rasmi kutoka Japani.

Alizaliwa Manzini kama mtoto wa mfalme Sobhuza II na mmoja wa wake zake wadogo, Ntfombi Tfwala.[2]

Alipokea ufalme tarehe 25 April 1986 akiwa na umri wa miaka 18. Wakati ule alikuwa mfalme mwenye umri mdogo zaidi duniani. Anatawala pamoja na mama yake Ntfombi Tfwala, ambaye sasa ni Mama wa Mfalme (Ndlovukati), akitawala kama mfalme mwenye mamlaka kubwa ndani ya katiba ya ufalme.

Mswati III ni maarufu kwa kuendeleza mila ya kuwa na wake wengi ambao mwaka 2020 walikuwa 15.[3]

Siasa zake, pamoja na maisha yake tajiri katika nchi maskini imesababisha upinzani ndani ya Eswatini na ukosoaji wa kimataifa.[4]

Marejeo

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.