Mlinzi mzamaji
Jenasi ya ndege wadogo wa bahari From Wikipedia, the free encyclopedia
Jenasi ya ndege wadogo wa bahari From Wikipedia, the free encyclopedia
Walinzi wazamaji ni ndege wadogo wa bahari wa jenasi Pelecanoides, jenasi pekee ya familia Pelecanoididae. Wataalamu wengine huwaainisha katika familia Procellariidae (walinzi), lakini walinzi wazamaji ni wadogo kuliko walinzi wengine, wana mabawa mafupi na mirija ya pua inaelekea juu badala ya mbele. Wanatokea bahari za kusini na huzamia kabisa ili kuwakamata gegereka wadogo hasa (krili, kopepodi na amfipodi) na samaki na ngisi wadogo pia. Majike hulitaga yai moja tu ardhini katika makoloni kwenye visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Kwa kawaida huyatembelea makoloni yao usiku kuzuia shakwe-waporaji.
Mlinzi mzamaji | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mlinzi mzamaji mdogo (Pelecanoides urinatrix) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.