Walinzi ni ndege wa bahari wa familia Procellariidae. Spishi za jenasi Macronectes huitwa Kwazi-bahari pia. Walinzi wanafanana na albatrosi. Kwa hivyo rangi zao zinatofautiana kutoka nyeupe kabisa kupitia nyeupe na kijivu au kahawia mpaka mwili wote mweusi. Wana domo kubwa lenye ncha kwa umbo la kulabu, lakini mirija miwili ya pua inaungana juu ya domo; ile ya albatrosi haiungani.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Mlinzi |
Mlinzi mkia-kabari |
Uainishaji wa kisayansi |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 16:
- Aphrodroma Olson, 2000
- Ardenna Reichenbach, 1853
- Bulweria Bonaparte, 1843
- Calonectris Mathews & Iredale, 1915
- Daption Stephens, 1826
- Fulmarus Stephens, 1826
- Halobaena Bonaparte, 1856
- Macronectes Richmond, 1905
- Pachyptila Illiger, 1811
- Pagodroma Bonaparte, 1856
- Pelecanoides Lacépède, 1856
- Procellaria Linnaeus, 1758
- Pseudobulweria Mathews, 1936
- Pterodroma Bonaparte, 1856
- Puffinus Brisson, 1860
- Thalassoica Reichenbach, 1853
|
Funga
Kama albatrosi, walinzi huenda mbali sana wakiruka angani na spishi nyingi zinaweza kuzunguka dunia. Hawapigi mabawa sana baada ya kuruka, lakini wananyiririka kwa mabawa yaliyonyooshwa. Huwakamata ngisi, samaki na gegereka na hula takataka ya uvuvi na mizoga pia. Spishi za Puffinus na Calonectris huzamia ili kuyakamata mawindo na wanaweza kufika zaidi ya mita 50 chini ya maji. Spishi nyingine huyakamata mawindo kijuujuu. Spishi kadhaa za Pachyptila huchuja maji kwa domo pana lao ili kupata zooplanktoni.
Kwa kawaida malinzi huyatengeneza matago yao kwa visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Spishi nyingi huyatembelea makoloni yao usiku kuzuia shakwe-waporaji. Jike hulitaga yai moja tu kwa kawaida ndani ya kishimo.
- Aphrodroma (=Lugensa) brevirostris, Mlinzi wa Kerguelen (Kerguelen Petrel)
- Ardenna carneipes, Mlinzi Miguu-rangipinki (Flesh-footed Shearwater)
- Ardenna gravis, Mlinzi Mkubwa (Great Shearwater)
- Ardenna grisea, Mlinzi Kijivucheusi (Sooty Shearwater)
- Ardenna pacifica, Mlinzi Mkia-kabari (Wedge-tailed Shearwater)
- Bulweria bifax, Mlinzi Mdogo wa St Helena (Olsen's Petrel) imekwisha sasa (karne ya 16)
- Bulweria bulwerii, Mlinzi wa Bulwer (Bulwer’s Petrel)
- Bulweria fallax, Mlinzi wa Jouanin (Jouanin’s Petrel)
- Calonectris borealis, Mlinzi wa Cory (Cory’s Shearwater)
- Calonectris diomedea, Mlinzi wa Scopoli (Scopoli’s Shearwater)
- Calonectris edwardsii, Mlinzi wa Kaboverde (Cape Verde Shearwater)
- Daption capense, Mlinzi Kichwa-cheusi (Cape Petrel)
- Fulmarus glacialoides, Mlinzi Rangi-fedha (Southern Fulmar)
- Halobaena caerulea, Mlinzi Buluu (Blue Petrel)
- Macronectes giganteus, Mlinzi Mkuu au Kwazi-bahari Kusi (Southern Giant Petrel)
- Macronectes halli, Mlinzi wa Hall au Kwazi-bahari Kaskazi (Northern Giant Petrel)
- Pachyptila belcheri, Mlinzi Domo-jembamba (Slender-billed Prion)
- Pachyptila desolata, Mlinzi wa Kisiwa Desolation (Antarctic Prion)
- Pachyptila turtur, Mlinzi Hua (Fairy Prion)
- Pachyptila vittata, Mlinzi Domo-pana (Broad-billed Prion)
- Pagodroma nivea, Mlinzi Mweupe (Snow Petrel)
- Pelecanoides georgicus, Mlinzi Mzamaji wa Georgia Kusini (South Georgia Diving Petrel)
- Pelecanoides urinatrix, Mlinzi Mzamaji Mdogo (Common Diving Petrel)
- Procellaria aequinoctialis, Mlinzi Kidevu-cheupe (White-chinned Petrel)
- Procellaria cinerea, Mlinzi Kijivu (Grey Petrel)
- Pseudobulweria aterrima, Mlinzi wa Reunion (Mascarene Petrel)
- Pseudobulweria rupinarum, Mlinzi wa St. Helena (St. Helena Petrel) imekwisha sasa (karne ya 20)
- Pterodroma baraui, Mlinzi wa Barau (Barau’s Petrel)
- Pterodroma deserta, Mlinzi wa Desertas (Desertas Petrel)
- Pterodroma feae, Mlinzi wa Fea (Fea’s Petrel)
- Pterodroma heraldica, Mlinzi Mtabiri (Herald Petrel)
- Pterodroma incerta, Mlinzi wa Schlegel (Atlantic Petrel)
- Pterodroma lessonii, Mlinzi Kichwa-cheupe (White-headed Petrel)
- Pterodroma macroptera, Mlinzi Uso-kijivu (Great-winged Petrel)
- Pterodroma madeira, Mlinzi wa Madeira (Zino’s Petrel)
- Pterodroma mollis, Mlinzi Manyoya-mororo (Soft-plumaged Petrel)
- Puffinus assimilis, Mlinzi Mdogo (Little Shearwater)
- Puffinus bailloni, Mlinzi wa Baillon (Tropical Shearwater)
- Puffinus baroli, Mlinzi wa Barolo (Barolo Shearwater)
- Puffinus boydi, Mlinzi wa Boyd (Boyd's Shearwater)
- Puffinus mauretanicus, Mlinzi wa Baleari (Balearic Shearwater)
- Puffinus persicus, Mlinzi wa Uajemi (Persian Shearwater)
- Puffinus puffinus, Mlinzi wa Uingereza (Manx Shearwater)
- Puffinus yelkouan, Mlinzi wa Yelkouan (Yelkouan Shearwater)
- Thalassoica antarctica, Mlinzi wa Antakitiki (Antarctic Petrel)
Streaked shearwater
Northern fulmar
Salvin's prion
Peruvian diving petrel
Black petrel
Westland petrel
Tahiti petrel
Bermuda petrel
Cook’s petrel
Black-capped petrel
Bonin petrel
Mottled petrel
Magenta petrel
Kermadec petrel
Black-winged petrel
Buller’s shearwater
Fluttering shearwater
Hutton's shearwater
Christmas shearwater
Short-tailed shearwater