From Wikipedia, the free encyclopedia
Detepwani ni ndege wa nusufamilia Cerylinae katika familia Alcedinidae. Spishi kubwa zinaitwa mkumburu au zumbulu. Wanafanana na midiria lakini spishi nyingi ni wakubwa zaidi na zote zina kishungi. Kwa kweli baina ya spishi hizi kuna zile kubwa kabisa za familia hii, lakini American pygmy kingfisher ni mdogo sana. Takriban spishi zote zina rangi ya majani ya metali mgongoni na nyekundu kidarini, lakini detepwani wa kawaida ni mweusi na mweupe tu.
Detepwani | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Detepwani hubobea katika kukamata samaki lakini hula gegereka, vyura na wadudu pia. Huchimba tundu katika ukingo wa mto ambalo ndani lake jike huyataga mayai 2-5.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.