Mitalojia (kutoka Kiingereza metrology) ni elimu ya upimaji[1]. Inalenga kuweka msingi kwa maelewano kuhusu vizio na matumizi yake ambayo ni jambo la msingi kwa shughuli za kimataifa.

Makala hii kuhusu "Mitalojia" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Jina

Neno limeundwa na "mita" (kipimo cha kimataifa cha umbali; kiasili Kigiriki μετρον) na "lojia", ambayo ni kiambishi kinachotaja sayansi au elimu ya jambo fulani[2]

Asili

Asili ya sayansi ya upimaji ya kisasa ilipatikana wakati wa mapinduzi ya Kifaransa. Wakati ule wingi wa vizio vya urefu vilivyokuwa kawaida, mara nyingi kwa kutumia vizio vya kimwili[3], wataalamu walipendekeza kutumia kizio kilichorejelea chanzo cha kimazingira yaani sehemu ya mzingo wa Dunia. Hii iliunda mfumo wa vizio vilivyokadiriwa kidesimali mnamo mwaka 1795. Mfumo huo ulianza kutumiwa pia na nchi nyingine na hatimaye kuleta mfumo wa vipimo sanifu vya kimataifa[4].

Matawi ya mitalojia

Wataalamu wa mitalojia huangalia hasa mambo matatu:[5][6]

1. Ufafanuzi wa vizio vya upimaji. Huu unahusu hasa kurejelea vizio vya upimaji kwa vizio vya kifizikia, tofauti na vizio vya kimazingira kama awali. Mfano mita ilifafanuliwa kiasili kama sehemu moja ya milioni ya umbali kutoka ncha ya kaskazini hadi ikweta. Baadaye imetambulikana kwamba umbo la Dunia si tufe kamili, umbali kati ya ncha hiyo na ikweta ni tofauti kutegemeana na sehemu unapopimwa. Hivyo umbo la Dunia halifai tena kwa ufafanuzi wa kizio sahihi. Wataalamu walitafuta ufafanuzi wa kifizikia ambao hautegemei vizio vinavyoweza kubadilika. Mwaka 1983 Kongamano la 15 la Uzani na Vipimo (General Conference on Weights and Measures; kifupi: CGPM) uliamua kufafanua mita kulingana na kasi ya nuru ikiwa sawa na umbali unaopitiwa na nuru katika sehemu ya 1/299 792 458 ya sekunde moja[7].

2. Kuhakikisha na kutathmini matumizi ya vizio hivi katika tasnia na biashara

3. Matumizi ya vizio vya upimaji katika sheria za nchi na za kimataifa.

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.