Mbayuwayu au vijumbamshale ni ndege wa familia Hirundinidae. Spishi nyingine zinaitwa kinega au kizelele. Wanafanana na teleka lakini hawa wamo katika oda yao yenyewe Apodiformes. Mbayuwayu wana miguu mifupi kama teleka lakini mabawa yao ni mafupi zaidi na spishi nyingi zina rangi kama nyekundu, buluu na/au zambarau. Hutua mara kwa mara. Hukamata wadudu wakiruka angani.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Mbayuwayu |
Mbayuwayu michirizi mdogo |
Uainishaji wa kisayansi |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 19:
- Alopochelidon Ridgway, 1903
- Atticora Boie, 1844
- Cecropis Boie, 1826
- Cheramoeca Cabanis, 1850
- Delichon Horsfield & Moore, 1854
- Haplochelidon Todd, 1929
- Hirundo Linnaeus, 1758
- Neochelidon P.L. Sclater, 1862
- Notiochelidon S.F. Baird, 1865
- Petrochelidon Cabanis, 1850
- Phedina Bonaparte, 1855
- Progne Boie, 1826
- Psalidoprocne Cabanis, 1850
- Pseudhirundo Sundevall, 1850
- Pseudochelidon Hartlaub, 1861
- Ptyonoprogne Reichenbach, 1850
- Riparia T. Forster, 1817
- Stelgidopteryx S.F. Baird, 1858
- Tachycineta Cabanis, 1850
|
Funga
Spishi kadhaa huyataga mayai yao ndani ya mashimo asilia au matundu yaliyoachwa na vigong'ota. Spishi nyingi nyingine hulichimba tundu lao katika maada isiyo gumu k.m. ukingo wa mto. Spishi za jenasi Hirundo, Ptyonoprogne, Cecropis, Petrochelidon na Delichon hulijenga tundu lao la matope kupambana na ukuta wa jabali au jengo kwa kawaida karibu na sehemu inayochomoza kama paa la jengo. Jike huyataga mayai 2-5.
- Cecropis abyssinica, Mbayuwayu Michirizi Mdogo (Lesser Striped Swallow)
- Cecropis cucullata, Mbayuwayu Michirizi Mkubwa (Greater Striped Swallow)
- Cecropis daurica, Mbayuwayu Kiuno-chekundu (Red-rumped Swallow)
- Cecropis domicella, Mbayuwayu Magharibi (West African Swallow)
- Cecropis semirufa, Mbayuwayu Tumbo-jekundu (Red-breasted au Rufous-chested Swallow]])
- Cecropis senegalensis, Mbayuwayu Mkubwa (Mosque Swallow)
- Delichon urbicum, Mbayuwayu-kaya (Common House Martin)
- Hirundo aethiopica, Mbayuwayu Habeshi (Ethiopian Swallow)
- Hirundo albigularis, Mbayuwayu Koo-jeupe (White-throated Swallow)
- Hirundo angolensis, Mbayuwayu wa Angola (Angolan Swallow)
- Hirundo atrocaerulea, Kizelele-milima (Blue Swallow)
- Hirundo dimidiata, Mbayuwayu Rangi-mbili (Pearl-breasted Swallow)
- Hirundo leucosoma, Mbayuwayu Mabawa-mabaka (Pied-winged Swallow)
- Hirundo lucida, Mbayuwayu Kidari-chekundu (Red-chested Swallow)
- Hirundo megaensis, Mbayuwayu Mkia-mweupe (White-tailed Swallow)
- Hirundo nigrita, Kizelele Koo-jeupe (White-bibbed au White-throated Blue Swallow)
- Hirundo nigrorufa, Mbayuwayu Mweusi-mwekundu (Black-and-rufous Swallow)
- Hirundo rustica, Mbayuwayu wa Ulaya (Barn Swallow)
- Hirundo smithii, Mbayuwayu Mkia-sindano (Wire-tailed Swallow)
- Petrochelidon fuliginosa, Mbayuwayu-misitu (Forest Swallow)
- Petrochelidon perdita, Mbayuwayu wa Bahari ya Shamu (Red Sea Cliff Swallow)
- Petrochelidon preussi, Mbayuwayu wa Preuss (Preuss's Cliff Swallow)
- Petrochelidon rufigula, Mbayuwayu Koo-jekundu (Red-throated Cliff Swallow)
- Petrochelidon spilodera, Mbayuwayu Kusi (South African Cliff Swallow)
- Phedina borbonica, Mbayuwayu-visiwa (Mascarene Martin)
- Phedina brazzae, Mbayuwayu wa Brazza (Brazza's Martin)
- Psalidoprocne albiceps, Mbayuwayu Kichwa-cheupe (White-headed Saw-wing)
- Psalidoprocne fuliginosa, Mbayuwayu-milima (Mountain Saw-wing)
- Psalidoprocne nitens, Mbayuwayu Mkia-mraba (Square-tailed Saw-wing)
- Psalidoprocne obscura, Mbayuwayu wa Fanti (Fanti Saw-wing)
- Psalidoprocne orientalis, Mbayuwayu Mashariki (Eastern Saw-wing)
- Psalidoprocne pristoptera, Mbayuwayu Mweusi (Black Saw-wing)
- Pseudhirundo griseopyga, Mbayuwayu Kiuno-kijivu (Grey-rumped Swallow)
- Pseudochelidon eurystomina, Mbayuwayu-mtoni (African River Martin)
- Ptyonoprogne fuligula, Mbayuwayu-mawe (Rock Martin)
- Ptyonoprogne obsoleta, Mbayuwayu-mawe Mweupe (Pale Crag Martin)
- Ptyonoprogne rupestris, Mbayuwayu-mawe wa Ulaya (Eurasian Crag Martin)
- Riparia cincta, Kinega Miraba (Banded Martin)
- Riparia congica, Kinega wa Kongo (Congo Martin)
- Riparia paludicola, Kinega Koo-kahawia (Brown-throated Martin)
- Riparia riparia, Kinega-mchanga (Sand Martin)
Mbayuwayu michirizi mkubwa
Mbayuwayu kiuno-chekundu
Mbayuwayu tumbo-jekundu
Mbayuwayu mkubwa
Mbayuwayu-kaya
Mbayuwayu Habeshi
Koo-jeupe
Mbayuwayu wa Angola
Mbayuwayu rangi-mbili
Mbayuwayu mabawa-mabaka
Mbayuwayu kidari-chekundu
Mbayuwayu mkia-mweupe
Kizelele koo-jeupe
Mbayuwayu mweusi-mwekundu
Mbayuwayu wa Ulaya
Mbayuwayu mkia-sindano
Mbayuwayu wa Preuss
Mbayuwayu koo-jekundu
Mbayuwayu kusi
Mbayuwayu-visiwa
Mbayuwayu-milima
Mbayuwayu wa Fanti
Mbayuwayu mweusi
Mbayuwayu-mawe
Mbayuwayu-mawe mweupe
Mbayuwayu-mawe wa Ulaya
Kinega koo-kahawia
Kinega miraba
Kinega koo-kahawia
Kinega-mchanga
White-banded swallow
Welcome swallow
Pacific swallow
Blue-and-white swallow
Brown-bellied swallow
Fairy martin
Streaked-throated swallow
Tree martin
Cliff swallow
Southern martin
Purple martin
Brown-chested martin
Southern rough-winged swallow
Northern rough-winged swallow
Mangrove swallow
White-winged swallow
Tree swallow
Violet-green swallow