From Wikipedia, the free encyclopedia
Maambukizo humaanisha kuingia kwa vidubini katika mwili geni kama vidubini hivi vinabaki, vinazaa na kuenea.
Maambukizo mara nyingi yanasababisha magonjwa yanayoitwa "magonjwa ya kuambukiza".
Si lazima kila ambukizo lisababishe ugonjwa, lakini magonjwa mengi ni magonjwa ya kuambukiza.
Kuna vidubini ambavyo vinaishi ndani ya mwili wa binadamu bila kusababisha hasara; kuna hata vidubini ambavyo ni muhimu kwa maisha na afya ya binadamu, kwa mfano bakteria nyingi zinazoishi ndani ya utumbo na kusaidia Mmeng'enyo wa chakula.
Lakini vingine vinaweza kusababisha hasara ama kwa sababu vinatoa sumu fulani au kwa sababu vinasababisha upinzani mkali wa mfumo wa kinga wa mwili ambao ni hatari kama idadi ya vidubini vyenye hasara ni kubwa sana au vikiongezeka haraka mno. Vidubini hivi vyenye uwezo wa kuleta hasara huitwa "pathojeni" (kutoka Kiingereza pathogen) yaani "sababishi mateso".
Ambukizo hutokea kama vidubini hatari vinaingia mwilini, kukuta mazingira vinapoweza kustawi na kuongezeka. Uvamizi wa vidubini vya nje kwenye mwili hutokea kila siku mara nyingi maana hewa tunaopumua, vitu tunavyogusa na chakula tunachokula, vyote vimejaa uhai kwa umbo la bakteria, virusi na kadhalika.
Mara nyingi mfumo wa kinga mwilini unatambua vidubini vya kigeni na kuviharibu bila sisi wenyewe kutambua hali isiyo kawaida. Lakini hata kama kinga wa mwili ni dhaifu, kama vidonda vya ngozi au utando telezi vinaruhusu kufika kwa vidubini mahali pasipo mfumo wa kinga imara, viini hivi vinaweza kusambaa na kuongezeka.
Hapo maitikio ya mfumo wa kinga yanaongezeka mara nyingi hadi kushinda wavamizi. Lakini itikio hili linakuja mara nyingi pamoja na dalili kali tunayoona kama dalili za ugonjwa k.mf. homa, maumivu na udhaifu. Katika hali hii ya kupambana na vidubini fulani mwili wote unaweza kudhoofika zaidi na kushambuliwa tena na viini vingine.
Hapo mashambulio yanaweza kushinda kinga ya mwilini na kusababisha hasara za kudumu hadi kifo. Siku hizi kuna madawa mbalimbali yanayosaidia mapambano dhidi ya vidubini hatari na hivyo kuwezesha mfumo wa kinga mwilini kumaliza wavamizi.
Njia za maambukizo zinatofautiana. Mafua husababishwa na virusi zinazoweza kutoka mwilini mwa mgonjwa anayekohoa au virusi zinaweza kuvuka umbali mdogo kwa hiyo watu wa karibu wanaweza kupokea vidubini hivi bila kumgusa mtu.
Maambukizo yanaweza kutokea kwa njia ya bakteria fulani zinazoweza kudumu nje ya mwili kwa mudu fulani; ilhali hazionekani inatosha kama mtu anagusa mahali penye bakteria hizi na baadaye kuingiza kidole mdomoni.
Virusi za UKIMWI ni za hatari kwa sababu ya ugumu wa tiba lakini ni dhaifu; haziwezi kudumu hata kidogo nje ya mwili, kwa hiyo zinamhitaji mtu mwenye Ukimwi kuwa karibu sana na mtu mwingine ili viowevu vya mwili kama damu au shahawa viweze kupita kutoka mmoja hadi mwingine bila kupoa.
Vidubini vinavyoweza kuingia katika mwili geni, kuenea mle na kusababisha hasara ni hasa
Lugha ya maambukizo imeanza kutumiwa pia nje ya biolojia kwa ajili ya vurugu katika kompyuta inayosababishwa kwa kuingia kwa programu ya kigeni zinazoitwa "virusi ya kompyuta".
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.