Lutu (kwa Kiebrania לוט - lōṭ; kwa Kiarabu لوط - lūṭ) alikuwa mtoto wa Haran, mdogo wa Abrahamu kadiri ya Biblia na Kurani, ambaye alimfuata kutoka Mesopotamia hadi Kanaani.
Katika Biblia habari zake zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo, ambapo sura ya 19 inatuchorea uovu wa watu ambao huko Sodoma ulizidi hata kumdai Mungu alipe kisasi.
Lakini kati yao mwadilifu Lutu akaokolewa, isipokuwa mke wake akaja kuadhibiwa kwa sababu aliangalia nyuma, kinyume cha agizo la Bwana (Lk 17:28-33).
Lutu alikuwa na sifa ya ukarimu maana aliwakaribisha wageni waliokuwa malaika ingawa yeye hakujua; kwa hiyo tusiache kufuata mfano wake huo.
Lutu ndiye baba wa makabila ya Wamoabu na Waamoni, waliokaa upande wa mashariki wa mto Yordani (leo nchini Yordani).
Viungo vya nje
- Our People: A History of the Jews – Abram and Lot at chabad.org
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lutu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.